Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari
Kituo cha kielelezo kwa taifa

Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari ni hospitali inayomilikiwa na wamisionari wa Shirika la Damu Azizi nchini Tanzania. Inawakilisha huduma bora na za kitaalamu kwa wahitaji.

Tibu, fariji, elimisha

Kutibu, kufariji, kuelimisha, si maneno tu

Kutibu, kuelimisha, kufariji si maneno tu bali ni dira inayotambulisha na kuelezea namna na tabia ya utume wa hospitali: sio tu sehemu ya kupata tiba bali ni sehemu ya kushiriki na kuelimisha.

Kituo rafiki kwa watoto

Mara nyingi ni kituo rafiki kwa watoto

Watoto na vijana mara zote huwakilisha msingi wa uwepo wa hospitali. Kila mwaka maelfu ya watoto wagonjwa ufikia huduma zetu katika kupata tiba ya maambukizi, majeraha, malaria na utapia mlo.

Idadi ya watu hospitalini

tazama kumbukumbu ya mwaka 2020

Je, unajua?

Wanaoingia

Uchunguzi wa kliniki

Vitanda

Uzazi

wagonjwa hospitalini

Upasuaji

Je, unaweza kufanya kazi katika hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari

Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari na Chuo cha Uuguzi ni familia kubwa: waajiriwa katika hospitali wanaishi pamoja na sisi katika utume wetu “kutibu, kuelimisha na kufariji” wale wote wanaokuja katika hospitali yetu. Kama unataka kujiunga na hospitali yetu tuma taarifa zako kwenda info@stgasparhospital.org

Je, unaweza kuishi katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari?

Kama unahitaji kuishi kwa siku chache katika eneo letu liitwalo Moteli, Hospitali ya “Mtakatifu Gaspari” ni chaguo sahihi kwako. Vyumba vya kulala mtu mmoja au wawili vinapatikana pamoja na chakula na mahali pa kufulia nguo kwa maombi maalumu. Moteli inapatikana ndani ya eneo la hospitali, eneo sahihi la kuishi na la upendo.

Je hospitali ni ya kiikolojia?

Katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari tunajitahidi kutunza mazingira na kuzalisha yale tunayoyahitaji kwa sababu hiyo, hospitali sio kwamba kuna gereji au karakana pekee bali pia kuna bustani ya mboga, bwawa la samaki, huduma ya kuchuja maji ya kunywa na umeme jua, na huduma za kufua na chakula.

Je michezo ni muhimu?

Michezo ni mojawapo ya miradi mikubwa katika hospitali yetu inayohusisha mpira wa neti, mpira wa pete, mpira wa miguu, mpira wa basket, viwanja vitano vya mpira wa miguu na uwanja wa mtakatifu Gaspari unaoendelea kujengwa, michezo hukusanya vijana pamoja.

Je hospitali ni chanzo cha furaha?

Utume wetu kama ilivyoelezwa katika dira yetu yaani “kutibu, kuelimisha na kufariji” lakini hii sio kwa madawa pekee bali pia kwa kuhusisha michezo ambayo ni msingi maalumuwa afya, hasa kwa watoto; ndiyo maana hospitli yetu imejikita katika eneo la michezo ambapo husaidia watoto kusahau kama ni wagonjwa kwa muda mfupi na baadaye hurudi kuwa watoto wa kawaida.

Tunachofanya

IDARA

Dawa ya jumla

Wodi ya upasuaji

Wodi ya wazazi

Wodi ya watoto

Idara ya misaada

Kwa nini kufanya kazi katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari?

Wataalamu wetu sio waajiriwa tu.

“Kufanya kazi katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari ni upendeleo kwa sababu inahusisha ushirikiano na mipango ya kuwajali wagonjwa na wahitaji. Na hii ni muhimu sana kwangu.”

Veronica R. Kijuu

Accounter

“Nilichagua kufanya kazi katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari kwa sababu ya uwepo wa ushirikiano wa kweli, ambao unasaidia maskini na wale wote wanaoishi vijijini na hawana msaada wa kupata huduma za kiafya..”

Dr. Adriano S. Chavala

MD - Daktari wa Jumla

“Napenda kufanya kazi katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari Kwa sababu ni eneo sahihi la kujifunza: hapa ninakutana na wagonjwa wengi kila siku.”

Dionis E. Bidiligi

Mtaalamu wa mionzi

“Kwa upande wangu kufanya kazi katika hopitali ya mtakatifu Gaspari inamaanisha kuwa na majukumu makubwa: kutanganza na kueneza upendo wa Kristo kwa kila mtu hasa kwa maskini, wagonjwa na waliotengwa.””

Sr. M. Imakulata Kilawe

MA - Msaididi wa madawa

Chuo cha uuguzu na utabibu cha
mt. gaspari

Chuo cha uuguzi cha mtakatifu Gaspari kilizinduliwa rasmi tarehe 4 Septemba 2016. Kinapatika ndani ya eneo la Hospitali ya Mtakatifu Gaspari na kila mwaka “hufundisha wauguzi wa kesho.”
Kuanzia Novemba 2, 2020, shule hiyo iliinuliwa kwa viwango vya Chuo, na kuwa Chuo cha Mtakatifu Gaspar cha Sayansi ya Afya na Ushirika.

St. Gaspar Hospital

P.O. BOX 12, Itigi - Singida - TANZANIA

Nambari za simu:

+255 755 454 040

E-mail:  

stgasparhospitalitigi@gmail.com

Link utili

- Sera ya afya

- Wamisionari wa Damu Azizi- General Curia

- Wamisionari wa Damu Azizi - Tanzania

- Wamisionari wa Damu Azizi - Italia