Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga katika chuo cha Uuguuzi cha Mt. Gaspar. Chuo hiki kinatoa kozi ya Uuguzi. Kozi hii ni ya miaka mitatu lakini unaweza kusoma kwa miaka miwili na kuhitimu kwa ngazi ya cheti. Chuo kipo chini ya Usimamizi wa Kanisa Katoliki kikiendeshwa na Shirika la Wamisionari wa Damu Takatifu ya Yesu. Kwa kuwa chuo kinaendeshwa na Kanisa Katoliki kinafuata maadili, kanuni na taratibu za kikatoliki. Chuo kimesajiliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii pamoja na NACTE. Chuo cha Uuguzi cha Mt. Gaspar kinapokea wanachuo wa jinsia zote (Wanaume na Wanawake).