Huduma ya Kiroho
kuwa karibu na wewe
Kuianza siku
Tunaanza na adhimisho la Misa takatifu (Kanuni ya Kirumi) kila siku asubuhi
Kuwa karibu
Mapadre wamisionari, masista na makatekista wanatoa huduma ya kuwasaidia, kuwasikiliza na kuwafariji wagonjwa.
Hospitali ya kila mtu
Kwa mahitaji, viongozi wa imani zingine hutoa huduma katika hospital yetu.

Huduma ya kiroho
Huduma ya kiroho ni kitu cha msingi sana hapa hospitlini kwetu, kwa heshima ya kila imani, kikanisa kidogo cha hapa hutumika kutoa huduma ya misa, na masakramenti.
Ushauri wa kiroho hutolewa na jumuiya ya mapadre waliopo hapa, mashirika ya masista wanaofanya kazi hapa na makatekista. Viongozi wa Kiroho wa madhehebu mengine wanaalikwa kuja kutoa huduma wakihitajika.