KUANZA TENA
Wodi ya upasuaji
Wakuu wa idara: Dr. Seif Nuru – Nz. Mbeleje Chimomo
WANAPATIWA UPASUAJI
Upasuaji ni moja kati ya shughuli kubwa katika hospitali yetu. Vyumba vya upasuaji vinahudima karibu wagonjwa 15 kwa siku.
VYUMBA VYA UPASUAJI
Hospitali ina vyumba 6 vya upasuaji: Vyumba vitatu vya upasuaji mkubwa na vitatu vya upasuaji mdogo. Kati ya vyumba hivyo chumba kimoja cha upasuaji mkubwa na kimoja cha upasuaji mdogo vimo katika wodi ya watoto.
wataalamu
Madaktari, wauguzi na wasaidizi katika idara ya upasuaji ni wenye weledi mkubwa: mafunzo yanaendelelea, kwa njia ya semina na kongamano mbali mbali na mafunzo maalum yatolewayo na madaktari kutoka nje ya nchi..
idara yetu
Idara ina vitanda rasmi 36, ingawa mara nyingi wagonjwa wanazidi idadi hii na inabidi kuwalaza katika maeneo mengine yenye nafasi.
Uimara wa idara hii ni weledi wa watumishi waandamizi madaktari na wauguzi. Wataalamu hawa hufanya kazi kwa kujitolea katika mazingira yenye changamoto nyingi. Huimarishwa pia katika elimu yao wanapopata nafasi ya kushiriki katika mafunzo au mikutano na wataalamu wenzao nchini au nje ya nchi.
Sehemu kubwa ya upasuaji unatokana na athari za ajali barabarani, dharura za viungo vya tumboni na vivimbe mbali mbali vya mwili. Kabla ya kufanya upasuaji chunguzi za kina (za maabara, picha za x-ray nk), hufanywa.
Kutokana na umuhimu wa mafunzo ya upasuaji tarehe 28 mei 2018 hospitali ya Mtakatifu Gaspari iliingia makubaliano na hospitali ya watoto (ya Bambin Gesu,Italia), ili kuimarisha zaidi upasuaji wa watoto, hususani katika nyanja ya plastic surgery. Watumishi wa hospitali ya Bambini Gesu watashiriki katika kutoa mafunzo kwa wataalamu wazalendo.

habari mpya
Tangazo la nafasi za masomo kwa kozi ya utabibu
Mkuu wa chuo wa sayansi ya afya na afya...
UP-GRADING 2020-2021
Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga...
PRE- SERVICE 2020-2023
Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga...