CHUO CHA UUGUZI na utabibu
St. Gaspar college of health and allied sciences
shule
Chuo cha uuguzi cha mtakatifu Gaspari kilizinduliwa rasmi tarehe 4 Septemba 2016.
Kama ndoto ya shirika la Wamisionari wa Damu Azizi wanaokiongoza pia. Kipo ndani ya eneo la Hospitali ya Mtakatifu Gaspari na kila mwaka “hufundisha wauguzi wa kesho.”
Kuanzia 2 Novemba 2020 shule hiyo iliinuliwa kwa viwango vya Chuo, na kuwa Chuo cha Mtakatifu Gaspar cha Sayansi ya Afya na Ushirika.
Maelezo
Utume wetu ni kufundisha wauguzi na wahudumu wa afya: kijamii, kiutu na kitaalamu.
Mipango
Chuo kimesajiliwa na kinatambulika kitaifa (NACTE)
Kujiunga
Shule inatoa kozi nne za masomo: cheti cha uuguzi, diploma ya uuguzi, cheti cha “dawa ya kliniki” na diploma ya “dawa ya kliniki”.
Nadharia na vitendo
Uimara wa chuo chetu ni msisitizo wa mazoezi ya vitendo zaidi ya nadharia wakati wa mafunzo.Maabara ya mazoezi iliyo ndani ya chuo husaidia sana katika mazoezi kabla ya wanafunzi kuja kwa wagonjwa mawodini.
Hospitali
Muungano mkubwa wa chuo na hospitali ya mtakatifu Gaspari huruhusu mafunzo kamili na ya kudumu, tunashukuru kwa mazoezi mengi na majitoleo ya wanafunzi kwa wataalamu.
Kozi za mafunzo
Mafunzo yatolewayo kwa wanafunzi yanastawishwa na kozi zitolewazo kwao. Kozi zinahusisha kuwahudumia wagonjwa mbalimbali na tafiti mpya juu ya mbinu za kitabibu.
Miaka tangu kuanzishwa
Wakufunzi na waalimu
Kozi zitolewazo
wamehitimu tangu kuanzishwa chuo
TAARIFA ZA CHUO
Ya kutumia wengi
Katika huduma ya jumuiya iliyoanzishwa 2006, chuo cha mtakatifu Gaspari kimejikita katika kuelimisha raia na wanafunzi. Hivyo wauguzi wana uwezo wa kushiriki katika huduma za jumuiya kwa wahitaji. Tunawashukuru wataalamu na watoa mafunzo.
Kuanzia 2 Novemba 2020, shule hiyo iliinuliwa kwa viwango vya Chuo, na kuwa Chuo cha Mtakatifu Gaspar cha Sayansi ya Afya na Ushirika.

Chuo cha Uuguzi na Utabibu cha mtakatifu Gaspari ni moja ya nyenzo katika kuimarisha hospitali yetu kwa sababu kinahusisha utoaji bora wa mafunzo yatolewayo na wakufunzi walio bobea katika nadharia na vitendo, mazingira safi na ushiriki wa wanafunzi.
Mkakati wa mafunzo
Utoaji wa elimu wa Shule ya Uuguzi ya Mtakatifu Gaspar inajumuisha njia nne tofauti: ya kwanza kupata cheti cha uuguzi (miaka miwili); ya pili kwa kupata diploma ya muuguzi; ya tatu kwa cheti katika dawa ya kliniki (miaka 2) na ya nne kwa diploma katika dawa ya kliniki (miaka 3).

Diploma ya uuguzi
Diploma ya uuguzi haitoi mafunzo kwa wale waliobobea bali kwa wote hata viongozi wa idara. Moyo wa kuanzisha na kugundua, ujuzi kinadharia na kivitendo, ujuzi wa kimahusiano na mpango kazi wa pamoja kwa wahitimu.
Kujiunga na chuo
Mwanafunzi mtarajiwa anaweza kutokea shule au kazini. Inategemea aina ya kozi unayotaka (cheti au diploma).
Kanuni lazima kuzingatiwa katika kujiunga.
Katika elimu ya sekondari waweza kujiunga na kwa ajili ya diploma, ukitokea kidato cha nne au cha sita.

ukubaliwa kwenye kozi ya vyeti ya miaka miwili inahitajika kupata angalau kiwango cha D katika biolojia na kemia na D katika fizikia au hisabati; kwa kudahiliwa kwa diploma ya miaka mitatu, tathmini ya awali ya C katika biolojia na kemia na D katika fizikia au hisabati inahitajika.
Umadhubutu wa chuo chetu? Mafunzo ya kinadharia na kwa vitendo yaliyofungamanishwa pamoja.
Chuo cha mt. gaspar kimeshika nafasi ya tatu kitaifa kati ya shule….za uuguzi tanzania. hii ni kutokana na mafunzo yanayoendana na mtaara wa taaluma husika.
KWA NINI UCHAGUE SHULE YA UUGUZI na utabibu
YA MT. GASPARi?
Habari ya shule
Tangazo la nafasi za masomo kwa kozi ya utabibu
Mkuu wa chuo wa sayansi ya afya na afya shirikishi cha mt. Gaspari anawatangazia watanzania wote, wazazi/ walezi na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne au cha sita nafasi za masomo ya utabibu (diploma in Clinical Medicine) yanayo tarajiwa kuanza mwezi march, 2021....
UP-GRADING 2020-2021
Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga katika chuo cha Uuguuzi cha Mt. Gaspar. Chuo hiki kinatoa kozi ya Uuguzi. Kozi hii ni ya miaka mitatu lakini unaweza kusoma kwa miaka miwili na kuhitimu kwa ngazi ya cheti. Chuo kipo chini ya Usimamizi wa Kanisa Katoliki...
PRE- SERVICE 2020-2023
Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga katika chuo cha Uuguuzi cha Mt. Gaspar. Chuo hiki kinatoa kozi ya Uuguzi. Kozi hii ni ya miaka mitatu lakini unaweza kusoma kwa miaka miwili na kuhitimu kwa ngazi ya cheti. Chuo kipo chini ya Usimamizi wa Kanisa Katoliki...