Shughuli za kitaifa

Tangu kufunguliwa, mwezi wa tano 1989, hospitali ina idadi kubwa ya watumishi (madaktari bingwa na wasaidizi) ambao husaidia hospitali kwa utaalamu na uwezo wao. Misingi ya hali hiyo ya kusaidiana katika kutoa huduma imewekwa tangu miaka ya mwanzo wa hospitali kwa kiwango kikubwa cha kuwafundisha watumishi. Kwa sasa karibu kila mwajiriwa wa hospitali ya Mt. Gaspari ni mzalendo.
Kwa sasa kitu muhimu ni ushirikiano kati ya watanzania na Hospitali ya watoto ya “Bambin Gesu” iliyopo huko Roma, Italia. Hospitali hii huitwa “hospitali ya kipapa” ambayo ni hospitali maarufu kimataifa kwa matibabu ya watoto, na uchunguzi wa kina katika magonjwa ya watoto. Kwa sababu hiyo, kwa sasa pameweka makubaliano rasmi ya ushirikiano kati ya hospitali yetu na hospitali ya “Bambin Gesu”. Wameungana kwa mitazamo inayofanana katika usalama na afya za watoto. Wameamua kushirikiana ili kuleta uwepo wa haki ya kupata matibabu bora ya ya kisayansi na kwa utaalamu wa hali ya juu. Makubaliano yanaonesha kwamba miaka mitatu ijayo hizi hospitali mbili zitafanya kazi pamoja katika utekelezaji wa mradi huu wa ushirikiano unaotazamiwa kuimarisha matumaini kwa watoto wengi.
Kipekee, watumishi wa hospitali ya “Bambin Gesu” watafundisha watumishi wa hospitali ya Mt. Gaspari katika utaalamu makovu katika mwili yatonayo na majeraha ya moto na pia kurekebisha baadhi ya vilema vya kuzaliwa navyo kama vile midomo sungura na kadhalika. Huduma hii kitaalamu huitwa “plastic surgery”. Pia watatoa msaada katika kusoma na kutafsiri picha za mionzi na za ultrasound
Makubaliano hayo yamefanywa ili kufikia lengo la kufundisha na kuimarisha utaalamu na uwezo wa watumishi katika kuwahudumia watoto na kisha kuimarisha mazingira ya hospitali kwa ujumla. Madaktari kutoka Italia watakaribishwa katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari, na shirika litawahudumia kipindi chote cha utume wao.

I

Mafunzo

Mafunzo bora yatatolewa kwa madaktari na wasaidizi wao. Hatimae madaktari na watumishi wazalaendo wataendelea kuto huduma bila kuhitaji msaada wa madaktari kutoka nje.
I

Msaada

Katika Mradi mpya wa tele-medicine tutaweza kupokea msaada wa kusoma na kutafsiri picha na pia kujadili na madaktari kimataifa kuhusu matibabu.
I

Kwa matibabu

Uvumilivu na uwezo wa hizi hospitali mbili, vikichanganywa pamoja, vitaweza kuleta matumaini kwa watoto wote watakaohudumiwa.
\

Makubaliano na hospitali ya watoto

Makubaliano yamesainiwa tarehe 18 mwezi 5 mwaka 2019 kati ya “Bambin Gesu” (hospitali ya watoto) na hospitali ya Mtakatifu Gaspari. Makubaliano hutoa msaada wa kusoma utambuzi wa picha (na picha za CT-SCAN) na uwezakano wa kuwafunza watumishi wa Tanzania katika hospitali ya Bambin Gesù.

\

“Marafiki”

Katka miaka 30 ya kazi na utume katika hospitali yetu, marafiki wengi wa kutoka Italia wamekuwa wakija katika hospitali yetu mara nyingi kutoa utaalamu wao kama msaada. Urafili huo utaendelezwa tena katika mradi huu wa “plstic surgery”

\

Upasuaji wa plastiki

Makubaliano yaliyosainiwa mwaka 2018 hueleza kwamba watumishi wa kiitaliano wa hospitali ya watoto wangefundisha watumishi wetu katika plastiki na maxillo-upasuaji wa usoni, ambayo kwa sasa haipo Tanzania.

mahali

St. Gaspar Referral Hospital

P.O. 12 – Itigi (Singida)

 

email

info@stgasparhospital.org

nambari ya simu

(+255) 262540193

(+255) 755454040

St. Gaspar Hospital

P.O. BOX 12, Itigi – Singida – TANZANIA

Fax: +255 732 -960 744

Nambari za simu:

+255 755454040
+255 26 254 0193

E-mail:  

info@stgasparhospital.org

Hospitali

– Tovuti rasmi

Hospitali leo

Huduma maalum

Booking

Tusaidia

 

 

 

Link utili

Sera ya afya

Wamisionari wa Damu Azizi General Curia

Wamisionari wa Damu Azizi – Tanzania

– Wamisionari wa Damu Azizi – Italia