CT-scan
Kwa uchunguzi sahidi zaidi
Mawazo ya utambuzi
Kitengo cha CT-Scan kilianzishwa mwaka 2015 na sasa ni kimojawapo pia cha vivutio vya wagonjwa kuja Itigi katika hospitali yetu.
Kitengo cha CT- scan kinasaidia sana katika masuala ya uchunguzi katika majeraha ya yanayotokana na hajari za barabarani, magonjwa katika ubongo na sehemu zingine za mwili, utafiti katika saratani mbali mbali na magonjwa ya mishipa ya damu. Ni kipimo muhimu sana katika kuchunguza sehemu za ndani za mwil
Hutolewa an wataalamu waliopata mafunzo maalum. Tunashirikiana pia na wataalam wengine nje ya hospitali kwa njia ya ki-elekitroniki katika kusoma na kutafsiri picha za mgonjwa.

Mazingira rafiki kwa watoto
Mazingira katika chumba cha CT-Scan yamepambwa kwa picha za ukutani ili kuvutia na kupunguza taharuki hasa kwa watoto
Hakuna haja ya kuogopa
Machine kwa ajili ya uchunguzi na kupunguza msongo wa mawazo na hali ya kuogopa (claustrophobia)
Mashine ya kisasa
Yenye uwezo wa kuchukua picha 64 kwa wakati mmoja.Ni moja ya huduma hadimu inayopatikana katika hospitali chache hapa nchini. Ilianzishwa mwaka 2015
Mambo manne muhimu katika CT-scan yetu
Chumba kimepambwa ili kuwa rafiki kwa wagonjwa, hususani watoto; Wataalamu wa mionzi hukikagua mara kwa mara kuhakikisha usalama wa wagonjwa na mazingira; tunawasiliana na wataalamu wengine katika kutafsiri picha na huduma hupatikina muda wowote.
Usalama wa vifaa
Huduma ni masaa 24/7
Msaada wa kitaalamu
Usahihi wa matibabu

Mawasiliano
mahali
St. Gaspar Referral Hospital
P.O. Box 12 – Itigi (Singida)
Tanzania