UTAYARI WA KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA HUSAIDIA IDARA.
HUDUMA
NA MADAWA
HUDUMA NA MADAWA
Hospitali ni kama “mashine” kubwa. Hufanya kazi tu kama vyuma vyote huungana katika utume mmoja: kwa sababu hii, katika hospitali yetu hakuna tu idara 6 kubwa lakini pia ina idara nyingine za miundo mbinu ambazo huwezesha utekelezaji wa shughuli zote za hospitali.
Maabara
Maabara hushghulikia vipimo vya wagonjwa kimaabara kwa wagonjwa kwika idara zote 6. Maabara hupokea sampuli na kutoa majibu ya vipimo katika saa zote 24 za siku. Hii husaidia madaktari kufanya matibabu sahihi na kwa haraka.
Huduma nyinginezo za matibabu
Matibabu kwa njia ya mazoezi
Matibabu haya ni muhimu kwa mazoezi ya viungo kwa wagonjwa wengi baada ya matibabu ya upasuaji au ya dawa. Ni muhimu sana kwa watoto waliozaliwa na vilema, ya kuungua moto au majeraha mbali mbali.
Famasia
Famasia ni eneo ambapo madawa mbalimbali hutunzwa na kusambazwa katika idara tofauti. Katika famasia kuna wanataaluma na wasaidizi wanaotoa huduma kulingana na mahitaji.
Magonjwa ya meno
Chumba kwa ajili ya meno katika hospitali kinatoa huduma kila siku hata huduma za dharura. Wengi wa wagonjwa wanaofika katika idara ya meno wanakuwa na magonjwa ya kuambukiza katika meno au fizi. Wengi huja kwa kuchelewa na kwa hiyo meno yao yanang’olewa.
X-Ray na Ultrasound
Uchunguzi kwa njia ya x-ray au ultrasound husaidia sana katika uchunguzi wa magonjwa yanayohitaji picha kabla ya upasuaji au matibabu mengine. Mara nyingi ni muhimu sana kupata picha kabla ya kufanya upasuaji uliopangwa au wa dharura.
Magonjwa ya macho
Huduma ni ya muhimu na mara nyingi watu wanaoishi vijijini hawaipati, kwani bado haijapewa kipaumbele kikubwa. Katika kitengo cha macho wagonjwa hutibiwa maradhi mbali mbali ya macho na kupimwa uoni.
Uchangiaji wa Damu salama
Tukishawishika kwamba utamaduni wa zawadi hauna mipaka pia katika hospitali yetu tangu mwanzo kabisa tumeendeleza huduma ya uchangiaji damu ikiwa inashangaza kwa kuwa na wachangiaji wengi wanaojitolea.
Huduma ya madawa
Kitua cha unyweshaji dawa
Moja kati ya habari za hivi karibuni katika hospitali ya mtakatifu Gaspari ni mafanikIo ya kutengeneza maji hayo hapa hospitalini badala ya kuyaagiza kutoka mbali. Kimsingi kitengo hiki kinajihusisha kutengeneza aina mbalimbali za maji ya “drip” karibu chupa 30,000 kwa mwaka
Mochwari
Mochwari mpya ilifunguliwa 2018, kwa sasa ina vyumba vya ubaridi na meza kwa ajili ya kufanyia uchunguzi. Huduma hii inaruhusu maiti kuhifadhiwa kwa muda mrefu mpaka hapo familia itakapochukua mwili huo.
Maji salama ya kunywa
Tangu mwanzo wa utume katika nchi ya Tanzania ilikuwa tamaa ya wamisionari kuwapatia wagonjwa na wakazi wa eneo hili maji yaliyochujwa. Maji hayo kwa kiwango kikubwa yamepunguza maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya matumbo.
Jiko
Wagonjwa, ndugu, na wanaowatunza wana uwezo wa kujipikia chakula wawapo hospitalini, japo pia hospitali hutoa huduma ya chakula kwa maskini na wasio na waangalizi.
Chumba cha watoto na cha michezo
Kwa mtazamo kwamba mazingira ya hospitali huleta mwelekeo wa msongo wa mawazo hasa kwa watoto, iliamuliwa kutengeneza chumba chenye kumfanya mtoto aburudike na kucheza akiwa hospitalini.
TIMU KUBWA YENYE UTUME MMOJA!
Madaktari, wataalamu wengi na wafanyakazi wanahakikisha mazingira yanakuwa safi, kuendeleza ukarabati na umakini wa nyaraka.
MIRADI
WAAJIRIWA
WAGONJWA kila mwaka
VIPIMO VYA MAABARA kwa mwaka
HUDUMA KWA WATANZANIA
Utume wa hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari na Chuo cha Mafunzo ya Uuguzi unaeleweka kwa wote, watumishi wageni na wazalendo, kama utume wa kutoa huduma kwa watanzania unaoongozwa na haki ya kujali utu wa kila mtu.
WATU WENGI WENYE DHUMUNI MOJA
Katika hospitali ya Mtakatifu Gaspari tuna dhumuni moja: kutoa huduma bora kwa wote wanaohitaji. “tunapaswa kufanya mengi kwa haraka na vizuri” alisema Mtakatifu Gaspari
“Lazima tufanye mengi, vizuri na haraka”
Mt. Gaspari del Bufalo