Utume wetu
Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari inapaswa kuwahudumia watu walio pembezoni mwa jamii kwa kuwapatia huduma za kitabibu, elimu juu ya kujikinga na magonjwa mbali mbali; vyote hivi vikijikita katika misingi na kanuni za kikristo. Huo ni utume wetu. Hospitali yetu inataka kuwa kiini cha maelekezo mazuri ya huduma za kiafya.
Waganga wa Hospitali ya Mtakatifu Gaspari hutumia vifaa tiba vizuri na vya kisayansi kwa usahihi na ukamilifu. Dhumuni letu ni kuhudumia na kukuza utu kiroho na kimwili. Hospistali ya Mtakatifu Gaspari inastawisha mazingira bora, uponyaji, faraja, elimu, heshima na uwazi. Tunathamini ubunifu, ugunduzi, fikra pevu na kuweka katika matendo fikra mpya za matabibu. Kwa sababu hiyo tunathamini na kuinua uwezo wa madaktari na wafanyakazi mbalimbali.
Uponyaji
Mtu anayekuja Itigi anafahamu kwamba anaweza kufaidika na utaalamu huo wa kitabibu.
Faraja
Utume wetu unaweka kipaumbele kuwajali ndugu zetu katika machungu na maumivu yao.
Uelimishaji
Hapa Itigi kuelimisha kunamaanisha kuweka matumaini katika maisha yajayo kwa kutoa utaalamu wetu kwa kila mmoja.
Kanuni
Kadiri ya mafundisho ya kikristo, tunaamini kabisa kwamba kila mmoja ana utu na haki ya kupata huduma. Ndani ya hospitali yetu maisha ya kila mmoja yanathaminiwa na kutunzwa kwa ukarimu.
Utume
Tunahitaji kuwahudumia watu waliopo pembezoni na wote wanaohitaji msaada wa matibabu. Tunahitaji kutoa huduma bora za kitabibu.
Watumishi
Bendera ya hospitali yetu ni watumishi. Waajiriwa wetu hufanya utume wetu kuwa wao, huishi kikamilfu katika falsa hii ya utume.
mahali
St. Gaspar Referral Hospital
P.O. 12 – Itigi (Singida)
info@stgasparhospital.org
nambari ya simu
(+255) 262540193
(+255) 755454040