Historia yetu
Hospitali ya Mtakatifu Gaspari inatambuliwa, kusimamiwa na kufadhiliwa na Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu Tanzania, katika mkoa wa Singida eneo la Itigi.
Baada ya kuona uhitaji mkubwa kutoka kwa watu wa eneo hilo hospitali ilizinduliwa rasmi mnamo mwaka1989 na leo hii imekuwa kielelezo kimojawapo cha kitaifa katika (utoaji wa tiba, na elimu), kama kauli mbiu yake isemavyo.
Idadi kubwa ya madaktari na madaktari bingwa, wataalamu wa afya na marafiki zetu, wametumia ujuzi wao kusaidia hospitali katika utume wetu, kwa zaidi ya miaka 30.
Hospitali ya Mtakatifu Gaspari inawakilisha moyo wa CPPS katika Tanzania, hususani Itigi.
Ongezeko kubwa la vifaa vya hospitali limekuza hospitali kwa kiasi kikubwa tofauti na mwanzo. Katika miaka 30 majengo mengi yameongezwa, na kubadili muonekano. Hospitali hii ni mojawapo ya kazi kubwa sana za wamisionari wa Damu Azizi na inaperusha bendera yao. Kwa sababu ya utendaji wa hospitali yetu kwa miaka mingi utu na matumaini yameonekana katika vijiji mbalimbali vya jirani. Vijiji hivi pia vimenufaika na huduma za umeme na upatikanaji wa maji safi ya kunywa.
Huduma zingine za kijamii na usafi wa mazingira pia zimeanzishwa kwa sababu ya uwepo wa hospitali hii. Huu ni mfano wa kweli katika kueneza moyo wa matumaini katika Tanzania ijayo.
Idadi kubwa ya madaktari na madaktari bingwa, wataalamu wa afya na marafiki zetu, wametumia ujuzi wao kusaidia hospitali katika utume wetu, kwa zaidi ya miaka 30.
Ongezeko kubwa la vifaa vya hospitali limekuza hospitali kwa kiasi kikubwa tofauti na mwanzo. Katika miaka 30 majengo mengi yameongezwa, na kubadili muonekano. Hospitali hii ni mojawapo ya kazi kubwa sana za wamisionari wa Damu Azizi na inaperusha bendera yao. Kwa sababu ya utendaji wa hospitali yetu kwa miaka mingi utu na matumaini yameonekana katika vijiji mbalimbali vya jirani. Vijiji hivi pia vimenufaika na huduma za umeme na upatikanaji wa maji safi ya kunywa.
Huduma zingine za kijamii na usafi wa mazingira pia zimeanzishwa kwa sababu ya uwepo wa hospitali hii. Huu ni mfano wa kweli katika kueneza moyo wa matumaini katika Tanzania ijayo.
Utume ya C.PP.S.
Hospitali hii imejengwa na kuratibiwa chini ya ufadhili wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu.
Tangu 1987
Hospitali hii ilianza kama kituo cha afya ambacho ndicho kilicho zaa hospitali ya arufaa ya Mt. Gaspari
Mfano wa huduma za afya
Hospital yetu ni tumaini halisi kwa watu wote wanao izunguka hospital ina hata kwa watu walio nje ya Itigi.
Mwanzo
Wamisionari waliwasili katika eneo la Singida kwa mwaliko wa askofu mahalia, wamisionari waliamua kufungua dispensari kusaidia wagonjwa wa eneo hili. Ilikuwa mwaka 1988./p>
shirika la C.PP.S.
Shirika la wamisionari wa Damu Azizi ni jamii ya maisha ya kitume katika kanisa katoliki linaloundwa na wakleri na mabruda ambao uishi maisha ya kijumuiya. Wamekuwepo Tanzania tangu 1966.
Hospitali
Hospitali ilijengwa kando kando ya dispensari iliyokuwepo awali ambayo ilidumu kwa muda mfupi; ni sehemu ya kielelezo cha huduma za afya kwa mkoa wa Singida na Tanzania, ilifunguliwa 1989.
mahali
P.O. 12 – Itigi (Singida)
nambari ya simu
(+255) 262540193
(+255) 755454040