Hospitali ya leo

Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari ni hospitali ya kuigwa kitaifa. Ipo Tanzania eneo la Itigi katika mkoa wa Singida. Hospitali hii haitoi huduma kwa wakazi wa eneo hilo pekee bali hata kwa wanaotoka maeneo mengine. Mara nyingi wanakuja Itigi kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitabibu au wanakuja kutafuta tumaini la kutibiwa pale wanapokosa ufumbuzi wa matatizo yao katika hospitali zingine. Hospitali hii ipoumbali wa kilometa 164 Magharibi mwa jiji la Dodoma na kilometa 118 Kusini mwa mji wa Singida.
Kwa sasa Hospitali ina jumla ya vitanda 320 vilivyogawanywa katika idara kuu nne: idara ya upasuaji, idara ya uzazi na magonjwa ya kike, idara ya watoto na idara ya magonjwa mchanganyiko. Kuna pia idara ya wagonjwa wa nje (OPD), na pia vitengo vya vipimo mbali mbali vya uchunguzi wa magonjwa. Aidha kuna vitengo vya kiufundi (technical support units) vinavyosimamia miundo mbinu ya hospitali.
Kila mwaka hospitali huudumia zaidi ya watu 31,000 katika idara ya Wagonjwa wa Nje (OPD) na hulaza zaidi ya wagonjwa 6000. Maabara hufanya zaidi ya vipimo116,000.
Zaidi ya maabara hospitali ina vitengo vingine vya uchunguzi wa magonjwa kwa mashine za kisasa za X-Ray, ECHO (kipimo kikubwa cha moyo), CT-Scan, Ultrasound na Doppler kwa ajili ya picha mbali mbali. Huduma hizi zinatoa uwanja mpana katika uchunguzi wa magonjwa.
Hospitali haitibu tu wagonjwa, bali inajihusisha pia na hutoaji wa elimu kwa wagonjwa na watu wanaowasindikiza. Elimu juu ya afya ni muhimu sana kwa ajili ya kinga. Kwa sababu hiyo watu wengine hushirikishwa katika kupewa elimu ya kinga juu ya magonjwa mabali mbali yanayopatikana katika jamii iayozunguka hopitali.
Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari ni miongoni mwa hospitali bora zilizopo Tanzania. Mafanikio haya yamefikiwa sio tu kwa sababu ya kuwepo kwa vyombo vya teknolojia ya kisasa bali pia kwa majitoleoya wataalmu wa matibabu, ambao leo hii wengi wao ni wazalendo.
Chuo cha Uuguzi cha Mtakatifu Gaspari pia kina mchango mkubwa katika mafanikio hayo. Chuo hicho kina uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi 250 kwa mwaka na kuwasaidia kupata astashahada na stashahada za uuguzi. Mafunzo ni ya nadharia na vitendo. Wanafunzi hupata nafasi ya kushiriki na kuhudumia wagonjwa kwa vitendo katika hospitali.
Dhana ya hospitali yetu ni kwamba mtu hatakiwi kuhisi upweke au kutengwa; yaani kila mtu anatakiwa kuwa na ufahamu juu ya umuhimu wa afya na tiba.

I

Hospitali ya Itigi

Hospitali ni kituo cha kumbukumbu na mafundisho
I

Maeneo maalumu 5 ya kitabibu

Kwa sasa Hospitali ina jumla ya vitanda 320 vilivyogawanywa katika maeneo matano makubwa: idara magonjwa mchanganyiko, upasuaji, chumba cha uzazi, idara ya watoto na idara ya wagonjwa wa nje (OPD)
I

Moja kati ya hospitali 5 bora Tanzania

Moja kati ya hospitali bora hapa Tanzania kwa sababu ya umakini wa matibabu na mafunzo endelevu kwa watumishi.
\

Utekelezaji

Kila mwaka zaidi ya wagonjwa 31,000 hutibiwa katika kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD), zaidi ya 6000 hulazwa. Karibu vipimo 116,000 hufanyika maabara.

\

Nyenzo (vitendea kazi)

Zaidi ya hayo hospitali ina vipimo vingine muhimu vya uchunguzi.

\

Mafanikio

Dhima ya hospitali yetu ni kwamba mtu hatakiwi kuhisi upweke au kutengwa katika haki ya kutibiwa na kupona.

mahali

St. Gaspar Referral Hospital

P.O. 12 – Itigi (Singida)

 

email

info@stgasparhospital.org

nambari ya simu

(+255) 262540193

(+255) 755454040

St. Gaspar Hospital

P.O. BOX 12, Itigi - Singida - TANZANIA

Nambari za simu:

+255 755 454 040

E-mail:  

stgasparhospitalitigi@gmail.com

Link utili

- Sera ya afya

- Wamisionari wa Damu Azizi- General Curia

- Wamisionari wa Damu Azizi - Tanzania

- Wamisionari wa Damu Azizi - Italia