UTAYARI KATIKA JAMBO LOLOTE
IDARA YA MAGONJWA MCHANGANYIKO
Wakuu wa idara
Dr. Rajab Chimile – Nz. Elifaz Godfrey
64
vitanda
Idara ya Magonjwa Mchanganyiko (Internal Medicine) hushughulika na magonjwa yote ya watu wazima ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
19
wataalamu
Watumishi katika idara hii wana mafunzo yanayowawezesha kukabiliana na kujibu kila hitaji na hali katika magonjwa mbali mbali.
1310
HUPATA NAFUU
Wagonjwa hufika hospitalini na kupewa vitanda wodini, mara nyingi baada ya trauma (hasa wale wapatao ajali barabarani) au majeraha ambayo hayajapona.
Idara yetu
Hospitali ya Mtakatifu Gaspari Itigi ina wodi kubwa ya magonjwa mchanganyiko ambayo inapokea wagonjwa katika hali ya dharura au wanaokuja kupata uchunguzi zaidi kutoka sehemu hospitali zingine.
Kuna jumla ya vitanda 64 katika wodi hii.
Kiujumla wagonjwa wengi ni wa magonjwa ya kuambukiza hasa katika mifumo ya hewa, damu, kifua au figo, pia wa magojwa yasiyoambkiza kama vile kisukari na shinikizo la damu.
Malaria na upungufu wa damu pia hushamiri.
Idara pia ina sehemu mahususi kwa ajili kuwatenga watu wa magonjwa ambukizi, ambapo wagonjwa hawa pia hutibiwa bila unyanyapaa.
habari mpya
Tangazo la nafasi za masomo kwa kozi ya utabibu
Mkuu wa chuo wa sayansi ya afya na afya...
UP-GRADING 2020-2021
Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga...
PRE- SERVICE 2020-2023
Hongera kwa kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga...