CHUMBA CHA DHARURA
IDARA YA WAGONJWA
WA NJE
MASAA 24 YA DHARURA NA HUDUMA YA CLINIKI
MAPOKEZI YA MGONJWA
Mara mgonjwa anapoingia hospitali, anapokelewa na wauguzi wawili ambao hufuata itifaki maalum- wanatathmini hali ya mgonjwa,wanakuchukua na kurekodi vipimo vya msingi. Wakitambua mgonjwa anayehitaji matibabu ya haraka wanampeleka hima kwa daktari.


UCHUNGUZI WA KITABIBU
Baada ya triage mgonjwa asiyehitaji huduma ya dharura anapelekwa kufunguliwa jalida na anapelekwa kwa daktari kwa uchunguzi na vipimo.
Katika IDARA YA OPD kuna vyumba vitatu vya uchunguzi wa awali na matibabu. Kila chumba kina daktari ambaye huona wagonjwa na kuagiza vipimo vya awali kufanyika. Sampuli za vipimo huchukuliwa na kupelekwa maabara.
Kwa namna hii muda wa kusubiri unaweza kupunguzwa kwa kiwango kikubwa.
MATIBABU
Baada ya uchunguzi wa kitabibu na kupata matokeo ya vipimo vya awali, daktari anaweza kuamua kumtibu na kukamilisha matibabu ya mgonjwa pale OPD, au akampeleka katika kliniki ya dakatri bingwa kwa uchunguzi zaidi. Aidha anaweza kumlaza wodini mgonjwa liyezidiwa moja kwa moja kutokea OPD.
Mwaka 2018 wagonjwa 6178 (19%) kati ya wagonjwa 31450 waliopitia OPD ndio waliolazwa.

MAGONJWA MAKUBWA MATANO KATIKA MAHUDHURIO YA OPD
%
MAAMBUKIZI
%
MAJERAHA (AJALI, KUUNGUA...)
%
YA MALARIA
%
KIKOHOZI NA KICHOMI
%
MAGONJWA YA MATUMBO
VIONGOZI WA IDARA
Supervisors: dr. Hilda makule peter – nz. SR. DELPHINA RAPHAEL TEMU
MADAKTARI WETU
Kuna madaktari wanane ambao hupokezana zamu pale OPD. Madaktari hawa wanao uwezo wa kumudu magonjwa yote ya kawaida. Pia wana uwezo wa kuanzisha matibabu ya dharura kwa wagonjwa waliozidiwa. Hupeana zamu katika kutoa elimu kwa uma unaofika OPD kuhusu magonjwa mbali mbali na namna ya kujikinga nayo.
Wengi wa madaktari hawa ni vijana walio na uwezo wa kujifunza haraka.
ZAIDI ya 30000
wagonjwa HUINGIA OPD KILA MWAKA
WAUGUZI WETU
Katika OPD yetu tuna wauguzi 18 na wasaidizi wengine. Wote waathamini kazi yao ya kuhudumia wagonjwa wanaofika kutibiwa. Wanatenda kazi zao kwa umakini, kwa haraka na kwa kujituma.
Zaidi ya 6178
WAGONJWA HULAZWA KUPITIA OPD
WAFANYAKAZI MADAKTARI WETU
OPD ni kama hospitali ya ndani ya nyingine: msaada wa haraka, huduma makini, kwa namba kubwa ya wagonjwa. Kwa sababu hii, kando ya matibabu yetu na mzunguko wa wauguzi, muundo wetu pia una wasaidizi watano ambao hudhamini usafi, na wengine watano walioajiriwa huwahudumia wagonjwa kwa kuwasajili, mzunguko wao kwenye wodi na Nyanja ya kiuchumi.