MRadi wa TELEMEDICINe

Itasaidia kuwa na ujuzi na maarifa shirikishi

Telemedicine

Mradi wa Telemedicine unahusisha mawailiano kati ya madaktari kwa njia ya mtandao wakijadilina na kupeana ushauri katika kuchunguza na kumtibu mgonjwa.
Hii njia inaweza kusaidia kutoa tafsiri sahihi ya vipimo na kutoa matibabu stahiki kwa mgonjwa, hasa pale panapokuwa na utata. Mradi huu wa telemedicine ni mmoja wapo katika mbinu za kisasa za mawasiliano kati ya madaktari au mahospitali, ulioanzishwa katika hospitali ya Mt. Gaspari iliyopo Itigi. Mradi huu umefanikiwa kwa ushirikiano na makubaliano na shirika lisilo la kiserikali la GHT Onlus. Faida ya mradi huu itakuwa katika nyanja mbili. Mosi, wagonjwa wataweza kupata haraka majibu sahihi ya vipimo vyao na watapata matibabu stahiki. Pili, madaktari na wauguzi wa hospitali ya Mt. Gaspari watapata nafasi ya kujifunza na kupanua maarifa yao wakati wakishauriana na wataalam wenzao nje ya nchi. Huduma hii inapatikana muda wote hapa hospitalini.
P

Mradi mpya katika hospitali ya Mt. Gaspari

Mradi wa telemedicine ni mojawapo ya miradi ya hivi karibuni yenye kustawisha utoaji wa utaalamu mahiri katika hospitali ya Mt. Gaspari.
s

Huduma masaa 24 kwa siku 7

Huduma hii inapatikana kila siku ili kuwawezesha wagonjwa wetu kupata majibu sahihi ya vipimo vyao na kupata matibabu stahiki mapema iwezekanavyo.

Ushirikiano wa Kimataifa

Huu mradi unaendeshwa kwa ushirikiano na shirika la hiari la GHT Onlus.

“Hospitali ya ufundishaji”

Kufanya kazi na wataalamu wote kutoka pande zote za dunia huruhusu wafanyakazi wetu kutanua maarifa yao na kuongeza utaalamu.

Faida nne za telemedicine

Telemedicine siyo tu mpya, ni salama, inashirikisha, inasaidia, pia inapatikana kwa urahisi, kwa wagonjwa wetu wote.
s

Faragha na usiri

i

Ni mwendelezo wa mafunzo ya tiba

Inawasaidia wataalamu mabigwa kutua huduma bora zaidi

Huduma ya hali ya juu ya kizaza cha sasa

Contatti

Indirizzo

St. Gaspar Referral Hospital
P.O. Box 12 – Itigi (Singida)
Tanzania
Telefono
(+255) 262 540 193
Email
info@stgasparhospital.org

Richiedi un consulto