kila wakati upendo kwa mama 

wodi

ya uzazi

 

Wakuu wa wodi

Dr. Simon Mrema – Nz. Aurea Macha

36

vitanda

Wodi ya wazazi ni wodi ya matumaini. Kila siku watoto wachanga wapya huzaliwa, huangaza na kuanza safari mpya ya maisha.
19

wataalamu

Madaktari 2 wa uzazi na magonjwa ya kike, wauguzi 12 na wasaidizi 5 ambao hukakikisha kwamba kila mama anahudumiwa na kuelekezwa katika mazingira rafiki.
2063

WATOTO HUZALIWA

Kiwango cha vifo vya watoto wanaozaliwa wodini kimepungua kwa asili mia tisini na nane (98%) katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

idara yetu

Wodi ya uzazi imejikita katika maswala ya uzazi na magonjwa ya kike, na ina uwezo wa kutoa huduma kwa mama na mtoto anapokuja hospitalini kwa matatizo ya uja uzito au kujifungua. Wodi ina jumla ya vitanda vya kawaida 36.
Sehemu ya kujifungulia ina vitanda vinne vya kuangalia mwenendo wa uchungu na vitanda viwili vya kujifungulia. Vitanda vingine vinane ni kwa ajili ya magonjwa ya kike mbali na uzazi.
Madaktari mara nyingi hujikuta wakitoa huduma tofauti tofauti au za dharura zinazoendana na hali ya uja uzito kama vile kifafa cha mimba, maambukizi (sepsis) uzazi pingamizi,upungufu mkubwa wa damu na matumizi ya dawa za asili.
Kwa zaidi ya miaka 30 wodi ya uzazi imekuwa wodi kimkakati katika hospitali yetu. Vifo vya kina mama na watoto vimepungua kwa kwa asilimia 80 katika miaka mitano iliyopita.
Maendeleo mengi yamefanyika, japo bado kuna mahitaji makubwa ya maboresho.

habari mpya

St. Gaspar Hospital

P.O. BOX 12, Itigi – Singida – TANZANIA

Fax: +255 732 -960 744

Nambari za simu:

+255 755454040
+255 26 254 0193

E-mail:  

info@stgasparhospital.org

Hospitali

– Tovuti rasmi

Hospitali leo

Huduma maalum

Booking

Tusaidia

 

 

 

Link utili

Sera ya afya

Wamisionari wa Damu Azizi General Curia

Wamisionari wa Damu Azizi – Tanzania

– Wamisionari wa Damu Azizi – Italia